TETESI ZA USAJILI NDANI YA KLABU YA YANGA KUELEKEA MSIMU MPYA

TETESI ZA USAJILI NDANI YA KLABU YA YANGA KUELEKEA MSIMU MPYA

Clatous Chama (34) anamaliza mkataba wake na Yanga mwishoni mwa msimu huu.

Mazungumzo ya mkataba mpya hayajafanyika na anatarajia kuondoka. Chama amepata ofa mpya ya timu za nje ya Tanzania Possibly, anaweza akaondoka after Kariakoo Derby

Katika kikosi cha Al Hilal, jina la winga Jean Claude Girumugisha raia wa Burundi ndilo lililozungumzwa zaidi kutokana na kasi yake na umahiri wa kupiga mashuti makali akitokea winga ya kushoto ingawa anatumia mguu wa kulia

Inaelezwa Yanga inampigia hesabu Kirumugisha aliyezaliwa Septemba 18, 2004 ili kumjumuisha katika kikosi chake kuelekea msimu ujao

Al Hila wako tayari kumuuza winga huyo lakini wanataka dau la usajili lisilopungua Bil 3 za Kitanzania. Bado Yanga haijawasilisha ofa yake rasmi ili kufungua mazungumzo ya kumnasa ‘kiberenge’ huyo

Klabu ya Yanga ilishafunga hesabu kwa kumuongezea mkataba kiungo wake kiraka Maxi Nzengeli raia wa DR Congo, imefahamika

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo imebainisha kuwa Maxi alisaini mkataba wa miaka miwili mwezi Mei 2025, hivyo kinachoendelea sasa mitandaoni kuhusu mustakabali wake ni propaganda tu

Yanga wameanza mapema mchakato wa kuboresha kikosi chao ambapo taarifa za uhakika zimeeleza wako katika hatua nzuri ya mazungumzo na baadhi ya mastaa akiwemo straika hatari wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah ambaye amefunga zaidi ya magoli 11.

Sowah aliyejiunga na Singida kupitia dirisha dogo la usajili la mwezi Januari anatajwa kuwa straika hatari zaidi nchini kwa sasa kutokana na kasi yake ya kutupia kambani, akifikisha zaidi ya mabao 10 katika kipindi cha nusu msimu tu, tofauti na anaoshindana nao.

Taarifa nyingine ambayo imekuwa na moto kutoka ndani ya Yanga ni kuhusiana na Yanga kupokea ofa 3 zinazohitaji huduma ya straika wao, Clement Mzize ambazo ni JS Kabylie, Zamalek na Al Ittihad ya Libya huku ofa ya Zamalekh ikiwa ni kubwa kuliko.

Hii inakuja mara baada ya Yanga kufanya biashara ya kumuuza aliyekuwa kiungo wao, Aziz Ki kwa dola za marekani zinazokadiriwa kufikia 350k ambaye amejiunga na kikosi cha Wydad Athletic Club ya Morocco.

Lolote linaweza kutokea katika dili hili na huenda uongozi wa Yanga ukatoa taarifa rasmi ya kumuaga Mzize hivi karibuni, akiwa ni staa wa pili baada ya hivi karibuni kuagana na Mbukinabe, Aziz Ki aliyetimkia Wydad AC.

Kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho taarifa kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Yanga na Aucho. Ikumbukwe mkataba wa Yanga na Aucho unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Za ndaani nyingine kutoka kwa Wananchi ni kuwatayari Yanga wamemalizana na kiungo, Pacome Zouzoua  na wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na nahodha wao, Dickson Job kwenye mikataba mipya.

Yanga wamefanya mazungumzo na Dickson Job ili kusaini mkataba mpya, mkataba wa Job na Yanga unamalizika rasmi mwishoni mwa msimu huu na Job ametaja ofa yake na Yanga wameomba muda wa kuichakata kabla ya maamuzi ya mwisho kufanyika.

Yanga wanamuona Job kama mchezaji muhimu kwenye kikosi chao na Job anaiheshimu Yanga na kuipa kipaumbele cha kwanza. Siku kadhaa zilizopita Simba waliulizia upatikanaji wake na wakaahidi kupeleka ofa yao ya kwanza baada ya fainali ya CAF, ameeleza Hans.

Kufuatia uwezekano wa kuachana na Aucho inaelezwa Yanga wanaiwinda saini ya kiungo wa ulinzi wa Djoliba AC, Daba Diakite raia wa Mali. Yanga wanamsaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21ili kuweza kuwa mbadala wa Aucho ikiwa wataachana nae.

Diakite amebakiza siku chache ndani ya mkataba wake wa sasa, hivyo huenda akaondoka kama mchezaji huru. Msimu uliopita Manchester Utd walituma scout wao kumtazama Diakite, Benfica Lisbon nao walifanya hivyo na huku Africa Kaizer Chiefs na De Tunis wanamtaka kiungo huyo.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *