YANGA HAWAPOI HAWATAKI MCHEZO TAYARI MCHEZAJI HUYU YUPO MIKONONI MWAO

YANGA HAWAPOI HAWATAKI MCHEZO TAYARI MCHEZAJI HUYU YUPO MIKONONI MWAO

Mshambuliaji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Selestin Ecua, ameaga rasmi klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu wa 2024/25 na sasa tetesi zinamuhusisha moja kwa moja na Yanga ya Tanzania.

Kupitia salamu zake za kuagana alizochapisha mitandaoni, Ecua amewashukuru mashabiki, benchi la ufundi na uongozi wa ASEC Mimosas kwa kumpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake na kukua kisoka. Hii ni ishara tosha kuwa nyota huyo yuko tayari kwa changamoto mpya na kwa mujibu wa vyanzo vya karibu, mwelekeo wake ni Jangwani, Dar es Salaam.

Kwa kawaida, Ecue hutumika kama winga wa kulia, kushoto, kiungo mshambuliaji na hata mshambuliaji wa kati

Ecua aliibuka kama mmoja wa nyota waliobeba majukumu ya kikosi cha ASEC baada ya kuondoka kwa Karamoko Sankara, na kwa kipindi kifupi, aliweza kuwashangaza wengi kwa uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kupachika mabao muhimu katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Yanga inamuwania na huenda akachukua nafasi ya Jonathan Ikangalombo ambaye inaelezwa ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi kuendelea nae

Juzi wakati akihitimisha gwaride la Yanga kusherehekea mataji matano ya msimu uliomalizika, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema wanakwenda kufanya maboresho makubwa wakilenga kufanya vizuri zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Squid Game (S03) Ep4

MIENDELEZO YA MUVI HIZI NA NYINGINE DOWNLOAD APP YETU👇🏻👇🏻

App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MUVI BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *