BREAKING: BAADA YA NGOMA KUACHANA NA SIMBA HUYU HAPA MRITHI WAKE PALE MSIMBAZI

BREAKING: BAADA YA NGOMA KUACHANA NA SIMBA HUYU HAPA MRITHI WAKE PALE MSIMBAZI

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeingia sokoni kusaka mbadala wa kiungo mkongwe Fabrice Ngoma aliyeachwa hivi karibuni. Katika harakati hizo, jina la kiungo chipukizi wa Bravos do Maquis ya Angola, Higino Epalanga Kapitango, tayari limewasilishwa mezani kwa mabosi wa Msimbazi.

Kapitango (22), ambaye aliwavutia wengi kwa kiwango chake thabiti kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) msimu uliomalizika, ni miongoni mwa wachezaji walioibeba Bravos katika michuano hiyo licha ya kuwa walishindwa kufuzu robo fainali baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu.

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kupiga pasi sahihi na mashuti ya mbali, ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Bravos do Maquis licha ya umri wake mdogo.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu zimeeleza kuwa Simba tayari imeanza mazungumzo rasmi na wakala wa Kapitango, ikiwa ni hatua ya awali kuelekea kukamilisha usajili huo.

Imeelezwa kuwa benchi la ufundi linaamini Kapitango anaweza kuleta kitu tofauti katikati ya dimba la Simba, akiongeza kasi na umakini katika eneo hilo.

Simba inatarajiwa kuongeza viungo wawili kwenye dirisha hili la usajili wa kiangazi, ili kuziba nafasi za Ngoma pamoja na Augustine Okejepha ambaye pia amewekwa sokoni kwa sasa.

Usikose kutazama mechi zote za ulaya Live bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *