BREAKING: FIFA KUFANYA UCHUNGUZI DHIDI YA YANAYO ENDELEA KWENYE MICHEZO TANZANIA

Taarifa za uhakika kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ni kuwa Shrikisho hilo litachunguza mpira wa Tanzania katika kipindi cha miezi miwili iliyopita kutokana na migogoro ya kimaamuzi iliyotokea

FIFA imeomba taarifa kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya yale yaliyogubika migogoro hiyo ukiwemo unaohusisha mechi namba 184 ya ligi kuu

FIFA imesisitiza kupata ushirikiano kutoka kwa TFF ili kupata uhalisia wa mambo yote yaliyojitokeza

Hii inaweza kuwa sio hatua nzuri kwa mustakabali wa soka la Tanzania kwani kama itabainika kuna maamuzi hayakufanywa kwa kuzingatia muongozo wa Shirikisho hilo, Tanzania inaweza kufungiwa

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *