TAARIFA MPYA KUTOKA BODI YA LIGI

TAARIFA MPYA KUTOKA BODI YA LIGI

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko muhimu katika safu yake ya uongozi kufuatia kuondoka kwa viongozi wawili wakuu, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu waliotoka kwenye nafasi hizo kwa sababu tofauti mnamo Juni 13, 2025.

Katika hatua ya kuhakikisha utendaji wa bodi haukwami, TPLB imemteua Makamu Mwenyekiti wake, Nassor Idrissa β€˜Father’, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam FC, kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa bodi hiyo. Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Steven Mnguto, kujiuzulu rasmi kwa barua mwishoni mwa juma lililopita.

Kwa upande mwingine, nafasi ya Mtendaji Mkuu wa TPLB imejazwa kwa muda na Ibrahim Mwayela, aliyekuwa Meneja Fedha wa bodi hiyo. Mwayela atakaimu nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Almas Kasongo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia

Kupitia barua rasmi kwa klabu zote wanachama, TPLB ilieleza:

β€œBodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.

β€œKatika hatua nyingine, Meneja Fedha wa TPLB, CPA Ibrahim Mwayela ameteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), baada ya Almasi Kasongo kusimamishwa kazi mwishoni mwa juma lililopita. Bodi inatarajia ushirikiano wa dhati wa klabu yako kwa viongozi hao.”

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *