FABRICE NGOMA AACHANA NA SIMBA

FABRICE NGOMA AACHANA NA SIMBA
Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma amewaaga mashabiki baada ya mkataba wake wa miaka miwili na Wekundu hao wa Msimbazi kufika tamati
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ngoma ametoa ujumbe huo wa kuaga na shukrani
“Namshukuru kila mmoja ambaye alinifanya mimi kujisikia nipo nyumbani nikiwa Simba. Shukrani zangu ziende kwa Salim Abdallah βTry Againβ na Boss MO ambao walinileta mimi misimu miwili iliyopita.”
“Shukrani kwa kocha, wafanyakazi na wachezaji ambapo kwa pamoja tulishirikiana katika chumba cha kubadilishia jezi. Hatujaweza kuyafikia baadhi ya malengo yetu, lakini kumbukumbu zitasalia akilini mwangu na moyoni”
“Kwenu mashabiki wa Simba, ahsanteni kwa ushirikiano, msiiache hii timu, nyakati nzuri zinakuja hasa kwa kupitia kocha kama Fadlu. Ahsanteni na kila la kheriβ ameandika Ngoma
