SISI TUKO TAYARI WAJE TU – JOB

SISI TUKO TAYARI, WAJE TU – JOB

Nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Job amesema wachezaji wote wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi ili kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mfululizo

“Sisi kama wachezaji tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Simba, tunaamini utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kushinda ili kutetea taji letu”

“Tumekuwa na maandalizi ya kimkakati kuelekea mchezo huo, naamini kama tutafanya kwa usahihi yale tuliyoelekezwa mazoezini basi tutashinda”

“Tunafahamu ubora wa wapinzani wetu, tutacheza kwa tahadhari lakini muhimu kufuata maelekezo ya mwalimu ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu,” alisema Job

Yanga imejichimbia Avic Town kukamilisha maandalizi ya mchezo huo ambao ushindi utawahakikishia Wananchi kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo

Usikose kuitazama mechi hii ya  YANGA vs SIMBA LIVE  bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *