MATOKEO Yanga Vs Singida Black Stars Fainali CRDB CUP Leo Tarehe 29 June 2025

MATOKEO Yanga Vs Singida Black Stars Fainali CRDB CUP Leo Tarehe 29 June 2025
Yanga imefanikiwa kutetea taji la CRDB kwa msimu wa nne mfululizo wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar
Mabao ya Duke Abuya dakika 40 na Clement Mzize aliyepachika bao la pili dakika ya 50 yametosha kuihakikishia Yanga ushindi huo unaolirudisha taji la CRDB Jangwani kwa msimu mwingine
Singida Black Stars walitoa upinzani mkali kwa Yanga hata hivyo ni Wananchi waliotengeneza nafasi nyingi zaidi na pengine Mzize kama angekuwa makini angeondoka na mpira huku Pacome Zouzoua nae akikosa moja ya nafasi adimu
Ni taji la tano kwa Yanga msimu huu, hakuna mjadala, Yanga imekuwa na msimu bora sana
HONGERA WANANCHI…!






