TETESI: WACHEZAJI WATAKAO PEWA MKONO WA KWAHERI YANGA
TETESI: WACHEZAJI WATAKAO PEWA MKONO WA KWAHERI
Stephane Aziz Ki amejiunga rasmi na Wydad Athletic Club ya Morocco kwa dau la jumla la Sh2.9 bilioni. Hili ni moja ya dili kubwa kuwahi kufanyika katika historia ya usajili Tanzania. Aziz KI aliiwakilisha Yanga kwa mafanikio makubwa kwa misimu mitatu, na sasa anajiunga na Wydad kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa Dunia.
Jonas Mkude: Mkude ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza. Ametumika kwa dakika chache sana msimu huu, jambo linaloashiria kuwa huenda asirefushiwe mkataba wake unaomalizika mwisho wa msimu.
Clatous Chama: Kiungo huyu kutoka Zambia amekosa nafasi ya kudumu, akicheza kwa dakika 727 tu katika mechi 24. Ingawa alihusika kwenye mabao 16 (mabao 6, asisti 9), ushindani mkali kutoka kwa Zouzoua na wengine huenda ukasababisha kuondoka kwake na tayari inaripotiwa ameshapata timu kutoka nje ya nchi.
Yao Kouassi: Beki kutoka Ivory Coast amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha. Hadi sasa amecheza mechi saba pekee msimu huu. Uwezekano wa kuongezewa mkataba ni mdogo, hasa baada ya Yanga kumsajili Israel Mwenda aliyechukua nafasi yake lakini pia anaweza kubaki hii itatokana ripoti kamili ya jeraha lake.
Farid Mussa: Inaelezwa kuwa mchezaji Farid Mussa huenda akatolewa kwa mkopo kwenda moja timu za hapa hapa tanzania hii ni kutokana na ushindani wa namba yake katika kikosi cha Yanga na kutopata nafasi ndani ya kikosi cha Wananchi.
Kennedy Musonda: Alitua jangwani msimu wa 2022/2023 akitokea klabu ya Power Dynamo ya Zambia huenda akapewa mkono wa kwaheri hasa baada ya kukosa namba katika kikosi cha Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miloud Hamdi
Aziz Andambwile: Huenda naye akapewa mkono wa kwaheri hii ni kutokana na kupata nafasi finyu ndani ya kikosi cha Yanga
Kwa tetesi zaidi endelea kutembelea blog hii kila wakati

