MATCHDAY: KENGOLD 🆚 SIMBA SAA 10:00

Kikosi cha Simba leo saa 10 jioni kitashuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kumenyana na KenGold katika mchezo wa ligi kuu, mzunguuko wa 29

Ni katika moja ya mechi nane zitakazopigwa katika viwanja mbalimbali katika muda mmoja, saa 10 jioni

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na malengo ya kuzisaka alama tatu muhimu ili kuendelea kusalia katika mbio za ubingwa

Wapinzani wao KenGold itakuwa mechi ya kukamilisha ratiba kwa upande wao kwani tayari wameshashuka daraja

Pengine inaweza kuwa mechi nzuri kwa Simba sio kusaka alama tatu tu, pia kujaribu kujiongezea mtaji wa mabao

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema wamekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo na hawatawadharau wapinzani wao kwani ni timu ambayo haina cha kupoteza

Kikosi cha Simba kilitua mkoani Tabora mapema jana na jioni timu ikapata nafasi ya kukamilisha maandalizi yake katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Usikose kuitazama mechi hii live bure hapa hapa mwanajamii unachotakiwa kufanya ni kushea habari hii kwenye magroup yako ya whatsapp na facebook pia link ya mechi itawekwa kabla ya mechi kuanza



 

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *