HUYU HAPA MRITHI WA YAO KUOASSI PALE YANGA

HUYU HAPA MRITHI WA YAO KUOASSI PALE YANGA
Mlinzi wa kulia wa kimataifa kutoka Mauritania, Ibrahima Keita, ameagana rasmi na mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe, zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkataba wake kumalizika rasmi mnamo Juni 30.
Keita, ambaye aliitumikia TP Mazembe kwa misimu miwili, amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi hicho, hasa katika safu ya ulinzi upande wa kulia. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa pande zote zimeamua kuachana kwa makubaliano, huku nyota huyo akiwa tayari kuangalia changamoto mpya.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Keita alikuwa nchini Tanzania wiki mbili zilizopita, ambapo alikutana na viongozi wa Yanga SC. Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa mazungumzo kati ya mchezaji huyo na Wananchi yamefikia hatua ya mwisho, huku usajili wake ukitarajiwa kukamilika katika kipindi kifupi kijacho.
Yanga inahaha kutafuta mrithi wa Yao Kouassi, ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja hadi Disemba mwaka huu kufuatia upasuaji wa goti alioufanyiwa.
Ingawa klabu hiyo inakusudia kumuongezea mkataba Kouassi, haitamsajili katika dirisha lijalo ili kumpa muda wa kupona ipasavyo. Anatarajiwa kupewa nafasi ya kurejea kikosini mwezi Januari 2026 iwapo atakuwa amepona kikamilifu.
Usajili wa Keita unatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya Yanga kuimarisha safu ya ulinzi na kuhakikisha wanakuwa na mbadala thabiti wa muda mrefu. Uwezo wake, uzoefu wa kimataifa, na weledi aliouonyesha TP Mazembe na timu ya taifa ya Mauritania unamfanya kuwa chaguo sahihi kwa klabu hiyo inayojiandaa kwa mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Endapo dili hilo litakamilika, basi Keita atakuwa miongoni mwa sajili za maana kwa Yanga msimu ujao.
Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs DODOMA JIJI Live bure kupitia simu yako download App hii itakayokuwezesha kuitazama mechi live kwenye simu yako bure, app bado haijawekwa plsystore hivo utaidownload kama APK
