HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA KITAKACHO ANZA LEO DHIDI YA SINGIDA BS FAINALI

HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA KITAKACHO ANZA LEO DHIDI YA SINGIDA BS FAINALI
Leo ndio siku ya mwisho kufunga hesabu za msimu wa mashindano 2024/25 kwa mchezo wa fainali kombe la CRDB kati ya Yanga dhidi ya Singida Black Stars ukipigwa katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar
Mechi nyingine kubwa na aina yake itashuhudiwa visiwani Zanzibar siku nne tu baada ya mchezo wa dabi ya Kariakoo ulioamua ubingwa wa ligi kuu Yanga ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Simba na kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Hii itakuwa fainali ya tano mfululizo kwa Yanga katika michuano hiyo, Wananchi wakilisaka taji la nne mfululizo
Hata hivyo ni wazi haitakuwa mechi nyepesi, msimu huu Singida BS wamejipambanua kuwa timu imara wakifanikiwa kutinga fainali kwa kuiondoa Simba kwa ushindi wa mabao 3-1 katika hatua ya nusu fainali
Yanga na Singida BS zinakutana kwa mara ya tatu msimu huu Yanga ikipata ushindi mwembamba katika mechi mbili zilizopita ambazo zote zilikuwa za ligi
Mchezo unaokumbukwa zaidi ni ule wa duru ya kwanza ambao ulipigwa uwanja wa New Amaan Complex, Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0
Mchezo huo ulikuwa miongoni mwa mechi bora katika ligi kuu msimu uliomalizika. Ni wazi leo mashabiki wa soka watashuhudia fainali nyingine bora visiwani Zanzibar
Kikosi cha yanga kikitoka utakipata moja kwa moja hapa hapa mwanajamii endelea kuwa nasi wakati wote
Usikose kuitazama mechi hii ya YANGA vs SINGIDA BLACK STARS LIVE  bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK
BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE
