TETESI ZA USAJILI SIMBA 2025/2026

TETESI ZA USAJILI SIMBA 2025/2026
Kuelekea msimu ujao wa mashindano ya ndani na kimataifa, Klabu ya Simba SC imeanza kusuka safu mpya ya ushambuliaji, na macho yao kwa sasa yako CΓ΄te d’Ivoire kwa mshambuliaji machachari wa ASEC Mimosas, Celestin Ecua.
Ripoti kutoka ndani ya klabu zinasema kwamba Simba imeingia katika mazungumzo rasmi na wasimamizi wa Ecua, mchezaji mwenye miaka 23 ambaye kwa sasa yupo ASEC kwa mkopo kutoka Zoman FC.

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeingia rasmi katika mbio za kumuwania kiungo mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Agee Basiala, anayekipiga katika klabu ya AS Maniema Union.
Taarifa zinaeleza kuwa Wekundu hao wa Msimbazi wanataka kuimarisha safu yao ya kiungo cha ushambuliaji kwa kumleta Basiala, ambaye pia anaweza kucheza kama winga.

Simba, Yanga na Azam zote katika nyakati tofauti zimefanya mazungumzo na Fei Toto ili kuona uwezekano wa kumsaini kiungo mshambukliaji huyo wa Tanzania huku Simba na Yanga zikiongoza mbio, sasa je, Fei Toto Kusaini Simba au Yanga?
Kwa mujibu ya mwandishi na mchambuzi, Hans Raphael kuhusu Fei Toto kusaini Simba au Yanga? muda wowote kuanzia sasa tajiri wa Simba, Mo Dewji atafanya mazungumzo na kambi ya Fei Toto.
Tayari Mo ameomba kikao na kambi ya Feisal na ikumbukwe awali Simba walimpa Fei Toto ofa ya mkataba wa miaka mitatu, wenye thamani ya Tsh 600m kama (sign on fee).
Simba waliahidi kutoa tsh 400m mwanzo na tsh 200m kwenye msimu wake wa pili ofa ambayo ilikataliwa. Ikumbukwe mezani Fei ana ofa ya Tsh 750m na mshahara wa tsh 40 kutoka Yanga.
MAKUBALIANO YA YANGA NA AZAM
Mchambuzi, Hans anaendelea kusema kuwa makubaliano yaliyowekwa kati ya Yanga na Azam ni endapo Fei atajiunga na timu yeyote tofauti na Simba basi Yanga watapata 25% ya mauzo.
Kama Fei atajiunga na Simba basi Azam watatakiwa kuilipa Yanga Tsh 1B. Hiki ni kizungumkuti kwa Fei, ni vita ya Yanga na Simba lakini pia Azam wanataka kumbakisha na wamefanya mazungumzo naye.
Kwa tetesi zaidi endelea kutembelea blog hii kila sikuπͺπ»
