ITAZAME LIVE MECHI YA YANGA VS SIMBA LIVE HAPA

ITAZAME LIVE MECHI YA YANGA VS SIMBA LIVE HAPA

Wanasema usiku wa deni haukawii, hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imefika. Ni mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa leo saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni mechi namba 184 ambayo awali ilipaswa kupigwa March 08 lakini haikufanyika baada ya Simba kugoma kucheza maamuzi ambayo yalipelekea Yanga kuweka msimamo wa kutocheza tena mechi hiyo hadi wale waliohusika kukwamisha dabi hiyo wachukuliwe hatua

Baada ya kilio cha Yanga kusikilizwa hatimaye Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mnguto na Mtendaji Mkuu Almas Kasongo wakan’goka katika Bodi ya ligi na Yanga kuridhia kucheza mchezo huo katika tarehe nyingine tofauti na Juni 15 ambayo Bodi hiyo ilikuwa imeupangia mchezo baada ya kuahirisha March 08

Mechi ya leo inakwenda kufunga hesabu za msimu huu, timu itakayoibuka na ushindi inakwenda kubeba taji la ligi kuu

Hivyo ni kama fainali lakini Wananchi wakiwa na faida zaidi kwani ushindi au hata matokeo ya sare yatawapa ubingwa. Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 79 huku watani zao Simba wakiwa na alama 78

Yanga imepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo, ikianzia maandalizi yake visiwani Zanzibar na jana kuhitimisha katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuipa sapoti timu yao katika mchezo ambao Yanga haipaswi kupoteza ili kutwaa ubingwa

Kumekuwa na propaganda nyingi nje ya uwanja kutoka upande wa Simba lakini taarifa ya uhakika ni kuwa saa 11 jioni nyasi za dimba la Mkapa zitawaka moto wakati mafahari wawili wakichuana

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewahakikishia Wananchi kuwa kikosi chake kiko tayari na wanakwenda kupambana ili kushinda mchezo huo

Usikose kuitazama mechi hii ya  YANGA vs SIMBA LIVE  bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *