TFF YAJIBU MASWALI HAYA KUHUSU KUTUMIA WAAMUZI KUTOKA NJE YA NCHI

TFF YAJIBU MASWALI HAYA KUHUSU KUTUMIA WAAMUZI KUTOKA NJE YA NCHI

Katika kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga na Simba itakayochezwa kesho Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Nassor Hamduni, ametoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kuihusisha timu ya waamuzi kutoka Misri kusimamia pambano hilo.

Hamduni amesema kuwa uamuzi huo hauna shaka wala matatizo yoyote, bali ni sehemu ya ushirikiano wa kimichezo kati ya nchi mbalimbali. Ameeleza kuwa sababu kubwa ya hatua hiyo ni kukosekana kwa waamuzi waliopaswa kuchezesha mechi hiyo ambao wako nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo.

“Waamuzi waliopangwa hawakuwa nchini, na hatukuwa na muda wa kuwaandaa wengine kwa haraka kwa ajili ya mechi kubwa kama hii. Hivyo tumeona ni sahihi kushirikiana na wenzetu kutoka nje,” alisema Hamduni.

Aidha, alibainisha kuwa ujio wa waamuzi kutoka nje si jambo la ajabu, bali ni fursa kwa waamuzi wa ndani kujifunza na kujiandaa kwa mechi za kimataifa.

“Kushirikiana katika michezo si jambo baya, na huu ni mwanzo tu. Hata waamuzi wetu wamekuwa wakipewa nafasi kwenda kuchezesha mechi nje ya nchi, basi na sisi pia tunakaribisha waamuzi kutoka nje, ni sehemu ya kujifunza,” aliongeza.

Hamduni pia amesisitiza kuwa mechi ya dabi ya Kariakoo ni tukio kubwa linalotazamwa na watu wengi duniani, hivyo inahitaji maandalizi ya hali ya juu na usimamizi wa kiwango bora.

Kwa maoni yake, hatua hiyo ni mwanzo wa maboresho katika usimamizi wa mechi kubwa, huku akisisitiza dhamira ya TFF kuendelea kuinua viwango vya waamuzi wa ndani kupitia mashirikiano ya kimataifa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Bodi mapema jana, Mwamuzi wa kati ni Amin Mohammed Amin Omar(Misri), ambapo atasaidiwa na mwamuzi msaidizi wa kwanza Mahmoud Ahmed Abo El Regal (Misri), Mwamuzi Msaidizi wa pili Samir Gamal Saad Mohamed (Misri), Mwamuzi wa akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour (Misri)

Kamishna wa mechi ni Salim Omary Singano (Tanga, Tanzania) na Mkaguzi wa waamuzi ni Alli Mohamed (Somalia)

Usikose kuitazama mechi hii ya  YANGA vs SIMBA LIVE  bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *