YANGA KUCHINJA NGAMIA KESHO KWA AJILI YA SUPU

YANGA KUCHINJA NGAMIA KESHO KWA AJILI YA SUPU
Baada ya kufanikiwa kutetea taji la ligi kuu ya NBC kwa msimu wa nne mfululizo, wakiwachapa watani zao Simba mabao 2-0 katika mchezo wa kiporo namba 184 uliopigwa jana Jumtano katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga haina muda wa kupoteza
Kesho Ijumaa kikosi kinatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar tayari kwa mchezo wa fainali kombe la CRDB utakaopigwa Jumapili, Juni 29 katika uwanja wa New Amaan Complex
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema timu inaelekea Zanzibar ikiwa na dhamira moja tu, kutetea taji la FA kwa mara ya nne
Dua maalum ya shukrani kufanyika Jangwani
Katika hatua nyingine, Kamwe amesema kesho Ijumaa, Makao Makuu ya Yanga, Jangwani itafanyika dua maalum ya shukrani baada ya kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu
Kamwe amesema duwa hiyo ni kwa ajiri y kushukuru na kuimbea timu iweze kushinda mchezo dhidi ya Singida Black Stars siku ya Jumapili
Kamwe amedokeza kuwa ul utaratibu wa kunywa supu utafanyika katika tukio hilo akitamba kuwa safari wanachinja Ngamia..!
“Msimu huu tumepitia mengi sana kama Klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio, Licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia. Viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama. Bila kusahau mchango wa Viongozi wote wa Matawi, Mashabiki na Wanachama tunasema Asante sana”
“Shukrani za kipekee ni kwa wachezaji wetu ambao walimwaga jasho na damu, benchi la ufundi wamejitoa kwa namna ya kipekee. Tunawapongeza pia wapinzani wetu wote 14 kwa kutupa ushindani wa kutosha”
“Lakini kwa kipekee tusiache kumshukuru mtanii kwa ubabaishaji, ubabaifu na propaganda. Yote hayo yamepelekea kutufanya sisi kuongeza umakini. Tuna furaha kubwa sana msimu huu”
“Mtakumbuka pale uwanja wa KMC, Msemaji wao alitangaza kuwa wao wanacheza mechi za Yanga. Ile kauli ilituamsha sana, wananchi Niwaambie ukweli, kauli ile ndiyo iliyokuwa kifo chao. Kubeba ubingwa ni jambo zuri, lakini mtani kutoka kapa ni furaha kubwa zaidi.”
“Kwenye sherehe za ubingwa tutaanza na dua ya kumshukuru Mungu. Asiyeshukuru kwa kidogo basi hata kwa kikubwa hawezi kushukuru. Hapo kesho tarehe 27, hapa makao makuu ya klabu tutaanza dua ya shukran na kuomba kheri kwa ajili ya mchezo ujao. Na baada ya hapo tutaweka historia kwa kunywa supu ya Ngamia,” alisema Kamwe
Usikose kuitazama mechi hii ya YANGA vs SINGIDA BLACK STARS LIVE  bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK
BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE
