USAJILI: Kudadeki! Simba wawafanyia umafia Yanga dhidi ya Mchezaji huyu

Kuelekea msimu ujao wa mashindano ya ndani na kimataifa, Klabu ya Simba SC imeanza kusuka safu mpya ya ushambuliaji, na macho yao kwa sasa yako Côte d’Ivoire kwa mshambuliaji machachari wa ASEC Mimosas, Celestin Ecua.
Ripoti kutoka ndani ya klabu zinasema kwamba Simba imeingia katika mazungumzo rasmi na wasimamizi wa Ecua, mchezaji mwenye miaka 23 ambaye kwa sasa yupo ASEC kwa mkopo kutoka Zoman FC.
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ameridhishwa na uwezo wa Ecua na ameidhinisha juhudi za kumleta Msimbazi kama sehemu ya maboresho ya safu yake ya ushambuliaji.
Ecua amekuwa na msimu mzuri tangu Januari 2025 akiwa na ASEC, akimaliza na mabao saba na asisti nne kwenye Ligi Kuu ya Ivory Coast, huku timu yake ikichukua nafasi ya pili.
Katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Ecua alionyesha thamani yake zaidi kwa kufunga mabao mawili hadi timu yao ilipofika robo fainali, ambako waliishia mikononi mwa RS Berkane.
Mshambuliaji huyo si wa kati tu pia ana uwezo mkubwa kutokea pembeni ya uwanja, akicheza kama winga. Uwezo huu wa kucheza nafasi nyingi ni moja ya sababu zinazomvutia Fadlu, ambaye amekuwa na changamoto ya kupata mshambuliaji mwenye versatility ndani ya kikosi chake.
Katika msimu huu, Ecua alimaliza akiwa mfungaji wa pili kwenye kikosi cha ASEC nyuma ya Salifou Diarrassouba aliyefunga mabao manane. Simba imepania kumsajili kama sehemu ya maboresho ya safu ya ushambuliaji kuelekea mashindano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao
Ikumbukwe pia Yanga wanamtaka mchezaji huyu kutoka Asec
