UFAFANUZI Kuhusu Ajira 33212 Kutoka UTUMISHI 2025

UFAFANUZI Kuhusu Ajira 33212 Kutoka UTUMISHI 2025
Rais Samia Suluhu Hassan jana ametoa kibali cha ajira kwa nafasi 33,212 za mwaka wa fedha unaoisha 2024/25 huku kada ya walimu ikipangiwa kupata nafasi 10,000 ambazo hazitafanyiwa usaili watachukuliwa kwenye Kanzidata.
Taarifa hizo zilidhibitishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene April 23,2025 akihitimisha hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Mwaka 2025/2026.
Katika taarifa hiyo Upande wa Kada ya WalimuΒ zitachukuliwa Nafasi 10,000 ambazo hazitafanyiwa usaili, hivo watachukuliwa kwenye Kanzidata.
Aidha Ajira hizo Zitakuwa Za Kada Mbalimbali Kama ifuatavyo
- Afya
- Walimu
- Kilimo
- Biashara
- Usafirishaji
- Wasaidizi Wa Ofisi Na Kumbukumbu
- Maendeleo Ya Jamii Na Ustawi Wa
- Jamii
- Wahasibu
- Wahandisi
- Na Kada Zingine
Angalia Video hapa Chini Kupata Taarifa zaidi.
