TAMISEMI Uchaguzi wa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 – Selform

TAMISEMI Uchaguzi wa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 – Selform
Wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano, huku 64,323 wakichaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu ya ufundi na Ualimu Mwaka huu 2025.
Jumla ya Wanafunzi 214,141 wakiwemo Wasichana 97,517 na Wavulana 116,624 wana sifa za kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya Elimu ya Ufundi ikijumuisha Wanafunzi 1,028 wenye mahitaji Maalumu.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo leo tatehe 6 June 2025 wakati akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo Mbalimbali nchini.
Aidha Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya elimu ya ufundi mwaka, 2025 inapatikana kwenye link hapa chini.
BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2025.
