TAARIFA MPYA KUTOKA YANGA MUDA HUU NI KUHUSU DUBE

TAARIFA MPYA KUTOKA YANGA MUDA HUU NI KUHUSU DUBE
Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Singida Black Stars leo katika mchezo wa fainali ya kombe la CRDB utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Dube amepewa mapumziko na benchi la ufundi ili aweze kupona kikamilifu majeraha ya nyama za paja
“Dube alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na maumivu. Ile ilikuwa mechi muhimu na uongozi ulifanya kila linalowezekana aweze kucheza na tuliona alikuwa na mchango wake katika dakika 45 za kipindi cha kwanza”
“Yeye amepewa mapumziko hivyo hayuko katika mipango ya mchezo dhidi ya Singida Black Stars”
“Yanga ina kikosi kipana, tunaamini wachezaji waliobaki watafanikisha malengo yetu ya kutetea taji la CRDB kwa msimu wa nne mfululizo,” alisema Kamwe
Dube aliumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons majeraha ambayo yalimfanya akose mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kabla ya kutumika kwa dakika 45 katika mchezo dhidi ya Simba
Mapumziko aliyopewa yatamsaidia kupona kabisa majeraha hayo na kurejea akiwa imara kwenye pre-season ya maandalizi kuelekea msimu ujao 2025/26
Usikose kuitazama mechi hii ya YANGA vs SINGIDA BLACK STARS LIVE  bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK
BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE
