TAARIFA MPYA KUTOKA SIMBA ASUBUHI HII

TAARIFA MPYA KUTOKA SIMBA ASUBUHI HII
Baada ya msimu wa 2024/25 kufikia tamati rasmi, uongozi wa klabu ya Simba SC umeamua kuwapumzisha wachezaji wake kwa muda wa wiki tatu. Mapumziko hayo ni sehemu ya kuwapa nafasi ya kurejesha nguvu baada ya kampeni ndefu ya mashindano ya ndani na kimataifa.
Simba inatarajiwa kurejea kambini katikati ya mwezi Julai 2025 ili kuanza maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Maandalizi hayo yanatarajiwa kuwa ya kiwango cha juu, hasa ikizingatiwa matarajio makubwa ya mashabiki na malengo ya klabu hiyo kwenye mashindano yajayo.
Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Fadlu Davids, tayari amewasilisha ripoti yake ya msimu iliyopita kwa uongozi wa klabu. Ripoti hiyo imeeleza maeneo mbalimbali yanayohitaji maboresho kwenye kikosi, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa au kuachwa.
Kwa upande mwingine, dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 1, ambayo ni siku ya Jumanne. Hii inamaanisha kuwa kuanzia tarehe hiyo, mashabiki wa Simba wataanza kupata taarifa rasmi za usajili, huku kila Mnyama akisubiri kwa hamu kuona maboresho yatakayofanywa kuelekea msimu mpya.
Wanasimba wamesisitiza kuwa matarajio yao ni kuona kikosi bora, imara na chenye ushindani mkubwa, kikijengwa kwa lengo la kurejesha makombe na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya CAF.
