SIMBA YAGOMEA MKUTANO WA MECHI NA WAANDISHI WA HABARI

SIMBA YAGOMEA MKUTANO WA MECHI NA WAANDISHI WA HABARI

Wanasema dalili ya mvua ni mawingu ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa Simba kugomea mkutano wa mechi unaohusu makocha na manahodha wa timu kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao umepangwa kupigwa kesho Jumatano, Juni 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kocha wa Yanga pamoja na nahodha wa timu hiyo walifika katika Mkutano huo lakini sio kocha Fadlu Davids wala nahodha Mohammed Hussein aliyefika kuzungumza

Akifunga Mkutano huo, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda alisema hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Simba kama watashiriki mkutano huo au la huku jitihada za kuwatafuta viongozi wa Simba zikigonga mwamba

“Licha ya jitihada tulizotumia ila mpaka kufikia muda huu baaada ya Mkutano wa Yanga na waandishi wa Habari. Klabu ya Simba mpaka kufikia muda huu bado hatuna majibu sahihi kama wanakuja au la. Tumejitahidi kuwatatuta lla hawajashika simu mpaka muda huu hivyo niwaambie ndugu zangu Mkutano wa Simba na waandishi wapo Habari haupo,” alisema Boimanda

Tangu mabadiliko ya ratiba ya kusogeza mbele mchezo huo yalipotangazwa, Simba haijajihusisha na hatua zote za maandalizi

Usikose kuitazama mechi hii ya  YANGA vs SIMBA LIVE  bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *