RASMI: Baada ya Kuwa kimya kwa muda Simba watoa tamko kuhusu Dabi kupigwa June 25

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema Simba inashiriki mashindano mbalimbali kwa kuzingatia taratibu za uendeshaji zinazopangwa na mamlaka husika

Mangungu amesema bodi ya ligi iliupangia mchezo namba 184 dhidi ya kupigwa Juni 15 lakini baadae wameusogeza mbele mchezo huo kupigwa Juni 25, Simba kama timu ya mpira wa miguu jukumu lake ni kucheza mpira

“Aliyetangaza mechi tarehe 15 ndiye aliyetangaza mechi tarehe 25 sisi hatujawahi kuhoji wala kujadili tulichokuwa tunasema ni utayari wetu wa kushiriki mashindano kulingana na mamlaka za mpira wa miguu zinavyotaka”

“Sisi tupo kwa ajili ya mashindano na kwa sasa mchezo ambao timu yetu inashiriki ni mpira wa miguu ambao una taratibu zake ambapo moja kati ya taratibu hizo ni mamlaka za mpira kutoa ratiba,” alisema Mangungu

Mangungu aliiwakilisha Simba waliopoitwa Ikulu mkoani Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk Samia Suluhu Hassan ambaye aliwakutanisha na viongozi wa klabu ya Yanga pamoja na mamlaka za soka nchini

Baada ya kikao hicho ndipo bodi ya ligi ikatangaza kusogeza mbele mchezo namba 184 ambao sasa utakuwa wa mwisho msimu huu

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *