NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya 3 2025

NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya 3 2025
NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya 3 2025

NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya 3 2025

TANGAZO NAFASI ZA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NGAZI YA TATU (LEVEL 3)

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inakaribisha maombi ya kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ngazi ya 3 kwenye vyuo vya VETA kwa mwaka 2025.

UCHUKUAJI NA URUDISHAJI FOMU
Fomu zitatolewa kuanzia tarehe 22 Aprili 2025 na mwisho wa kurudisha ni tarehe 20 Juni 2025.

SIFA ZA KUJIUNGA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NGAZI YA TATU (LEVEL 3)
Mwombaji anatakiwa awe na Cheti cha Taifa cha Ufundi Stadi (NVA Level 2) kinachotambuliwa na VETA.

UPATIKANAJI WA FOMU
Fomu zinapatikana katika vyuo vyote vya VETA na kwenye tovuti:
www.veta.go.tz

Malipo ya fomu ni Shilingi 5,000 (Elfu Tano tu) na italipwa wakati wa kurejesha fomu.4.

ADA KWA MAFUNZO YA NGAZI YA TATU

  • ADA YA KUTWA: Shilingi 60,000 kwa Mwaka.
  • ADA YA BWENI: Shilingi 120,000 kwa Mwaka.

Kwa Maelezo na Ufafanuzi zaidi, wasiliana nasi: VETA Makao Makuu,
12 Barabara ya VETA, 41104 Tambukareli,
S. L. P. 802, Dodoma
Barua pepe: info@veta.go.tz au pr@veta.go.tz Simu: +255 26 2963661

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *