NAFASI Za Kazi Africa Inland Church Tanzania

NAFASI Za Kazi Africa Inland Church Tanzania
Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga limekuwa likitoa huduma kwa watoto wanaotoka kwenye kaya maskini kupitia kituo cha Huduma ya maendeleo kamilifu ya Mtoto (Holistic Child Development Ministry) kwa kushirikiana na Shirika la Compassion International Tanzania (CIT).
Kanisa kupitia Program za maendeleo kamilifu ya mtoto linalenga kuwafungua watoto katika umaskini kwenye maeneo ya Kiroho, Kiuchumi, Kijamii na Kimwili (ambao ndio ujumla wa mtu), kwa shabaha ya kuwawezesha wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na wanaojitosheleza.
