NAFASI 4015 Za Aafisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II MDAs na LGAs

NAFASI 4015 Za Aafisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II MDAs na LGAs, Assistant Nursing Officer II Nafasi – 4015.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kutoa huduma za uuguzi.
- Kukusanya takwimu muhimu za afya.
- Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
- Kutoa huduma za kinga na uzazi.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka
miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la
Wauguzi na Wakunga Tanzania.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS B
