MSEMAJI WA SIMBA AHMED ALLY AVUNJA UKIMYA NA KUTOA UJUMBE HUU BAADA YA SIMBA KUBONDWA NA YANGA MARA 5 MFULULIZO

MSEMAJI WA SIMBA AHMED ALLY AVUNJA UKIMYA NA KUTOA UJUMBE HUU BAADA YA SIMBA KUBONDWA NA YANGA MARA 5 MFULULIZO

Baada ya ukimya wa siku mbili, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewapa pole Wanasimba kufuatia kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga juzi, matokeo ambayo yamekwenda sambamba na kupoteza ubingwa wa ligi

Hata hivyo Ahmed amewataka Wanasimba kutokata tamaa, kuendelea kuwa wamoja katika kuiunga mkono Simba kwani kilichokosekana msimu uliomalizika ni makombe tu lakini timu imepiga hatua

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;

“Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBC

Wana Simba tuepuke presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi

Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani.

Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31

Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na Dkk 45 za Kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu

Points tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita

Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu

Si mara ya kwanza Simba kukaa miaka minne bila Ubingwa , tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka Minne mfululizo.

Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau

Madrid amepoteza El Classico nne dhidi Barcelona tena kwa vipigo vya vikali lakini katu huwezi kuwaona wanajitukana

Sio mfano wa kujivunia lakini lazima tukubali nyakati hizi hutokea kwenye mpira

Pamoja na ukubwa wote Manchester United wanaenda mwaka wa 13 bila Ubingwa, Sitaki kutoa mfano wa Arsenal

Mifano hii itupe taswira kuwa hatuko peke yetu kwenye mapito ya namna hii na hata hawa wanaocheka sasa yapo magumu waliyopitia

Ombi langu wangu Wana Simba, tuwape nafasi viongozi wetu wafanye tathmini na baada ya hapo watupe muongozo tunaendaje mbele kuipambania Simba yetu

Heshima yetu itarudi kwa kushikamana na kusimama pamoja

Nguvu Moja!!!!!!!”

Usikose kuitazama mechi hii ya  YANGA vs SINGIDA BLACK STARS LIVE  bure kupitia simu yako  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *