MILIONI 500 ZAWEKWA MEZANI YANGA KUPATA USHINDI DHIDI YA SIMBA

MILIONI 500 ZAWEKWA MEZANI YANGA KUPATA USHINDI DHIDI YA SIMBA

Kuelekea mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, klabu ya Yanga imeweka msimamo mkali: ushindi ni lazima!

Katika kikao kizito kilichofanyika jana Jumatatu kabla ya safari ya kurejea jijini Dar es Salaam, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana kwa ajili ya kuweka malengo ya mwisho kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Mechi hiyo, ambayo imeahirishwa mara mbili kutoka Machi 8 na Juni 15, sasa itapigwa kesho, Juni 25, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11 jioni. Ni mchezo unaobeba hatima ya ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu huu, ambapo Yanga inaongoza kwa alama moja dhidi ya watani wao Simba.

β€œTumekutana na vijana tumewaambia maana halisi ya mchezo huu… huu si mchezo wa kawaida. Heshima ya viongozi wetu na mashabiki iko mezani, na kitu pekee tunachohitaji ni ushindi,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga.

Katika kikao hicho, wachezaji walipewa maagizo maalum ya kuhamasishana na kuweka akili zote kwenye mechi hiyo, ambayo huenda ikaamua bingwa wa msimu huu. Imeelezwa Mfadhili/Mdhaamini wa Yanga GSM ameweka mezani kitita kisichopungua Tsh Milioni 500 kwa ajili ya ushindi katika mchezo huo

Yanga, yenye pointi 79 baada ya mechi 29, haihitaji kupoteza mchezo huo ili kubeba taji. Simba wanafuatia kwa pointi 78, hivyo mechi hii ni fainali isiyo rasmi ya Ligi Kuu msimu wa 2024/25.

Kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es Salaam jana mchana tayari kwa maandalizi ya mwisho. Baada ya kuwasili bandarini, timu ilielekea moja kwa moja kambini Avic Town, Kigamboni

Usikose kuitazama mechi hii yaΒ  YANGA vs SIMBA LIVEΒ Β bure kupitia simu yakoΒ  download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure, pia App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MECHI HII LIVE BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *