MATCH DAY: TANZANIA PRISONS 🆚 YANGA LEO SAA 10:00

Mechi za mzunguuko wa 29 ligi kuu ya NBC zinapigwa leo katika viwanja mbalimbali ambapo mabingwa watetezi Yanga wako mkoani Mbeya kumenyana na Tanzania Prisons

Viwanja nane vitashuhudia timu 16 zikichuana mechi zote zikitarajiwa kuanza saa 10 jioni

Wananchi wakiwa ndio vinara wa ligi kuu, ni wazi watahitaji kushinda mbele Prisons ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji wanalolishikilia kwa misimu mitatu mfululizo

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema anauchukulia mchezo dhidi ya Prisons kama fainali akiamini kikosi chake kinahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa

Kwa upande wa Tanzania Prisons, timu hiyo inapambana kujiondoa katika eneo la kucheza play-off ikiwa na alama 30 katika nafasi ya 13

Hivyo mchezo huo unakutanisha timu ambazo kila moja ina malengo yake, Yanga ikihitaji kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi mbele ya watani zao Simba ambao watakuwa mkoani Tabora kumenyana na KenGold ambayo tayari imeshuka daraja

Ikumbukwe Yanga na Simba zinatofautiana alama moja katika msimamo wa ligi hivyo timu itakayofanya makosa ya kudondosha alama katika mechi hizi za mwisho itatoaa nafasi kwa mpinzani wake kwenye mbio za ubingwa

Usikose kuitazama mechi hii live bure hapa hapa mwanajamii unachotakiwa kufanya ni kushea habari hii kwenye magroup yako ya whatsapp na facebook pia link ya mechi itawekwa kabla ya mechi kuanza



 

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *