Hii hapa taarifa ya Prince Dube Baada ya kuumia jana

Hii hapa taarifa ya Prince Dube Baada ya kuumia jana
Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube jana alishindwa kuendelea na mchezo dhidi yaa Prisons baada ya kupata majeraha ya nyama za paja ‘hamstring’
Dube anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi kubaini ukubwa wa jeraha lake lakini ni wazi anaweza kukosa mchezo unaofuata dhidi ya Dodoma Jiji siku ya Jumapili
Majeraha hayo ni kama yamemtibulia Dube ambaye alikuwa katika mbio za kuwania tuzo ya ufungaji bora
Tunampa pole na kumtakia kila la kheri, apone haraka na kurejea katika majukumu yake
Get well soon Dube…!
