HAMDI AWAPANIA DODOMA JIJI AWATAJA WACHEZAJI WATAKAOUKOSA MCHEZO WA KESHO

HAMDI AWAPANIA DODOMA JIJI AWATAJA WACHEZAJI WATAKAOUKOSA MCHEZO WA KESHO
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema hawana nafasi ya kufanya makosa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Hamdi amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa
Hata hivyo amesisitiza mchezo hautakuwa mwepesi kwani kila timu inayocheza dhidi ya Yanga hupambana kwa kila namna kupata matokeo mazuri
“Mimi sitakuwa na maneno mengi kwa sababu mchezo dhidi ya Dodoma Jiji tunahitaji kushinda hatutaki kusikia sare au kupoteza”
“Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu kila timu inayocheza dhidi ya Yanga hupambana hadi tone la mwisho”
“Ni muhimu kwetu kushinda mchezo huu na tukifanikiwa nadhani tunaweza kuanza kufikiria ubingwa”
“Wachezaji wote wanafahamu jukumu lililoko mbele yao naamini watacheza kwa ari kubwa kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Hamdi
Akizungumzia hali ya kikosi, Hamdi amesema washambuliaji Prince Dube na Kennedy Musonda watakosekana lakini wachezaji wengine wote wapo
“Dube alipata majeraha madogo katika mchezo uliopita, tumekuja nae Zanzibar kwa ajili ya kuendelea kuimarisha afya yake, Musonda bado mgonjwa,” aliongeza Hamdi
Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs DODOMA JIJI Live bure kupitia simu yako download App hii itakayokuwezesha kuitazama mechi live kwenye simu yako bure, app bado haijawekwa plsystore hivo utaidownload kama APK
