Haji Manara aweka wazi Jambo hili kuhusu Pacome

Haji Manara aweka wazi Jambo hili kuhusu Pacome

Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara amesisitiza kauli yake kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Pacome Zouzoua, msimu huu atabeba tuzo ya mchezaji bora wa msimu ‘MVP’

Pacome jana aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons akifunga mabao mawili katika mchezo huo ambao baada ya dakika 90 kutamatika, alitangazwa nyota wa mchezo

Ilikuwa tuzo yake ya 7 ya nyota wa mchezo msimu huu akiwa mchezaji aliyeshinda tuzo hizo mara nyingi zaidi mpaka sasa

Manara alimtabiria Pacome kubeba tuzo hiyo hata kabla ya msimu huu kuanza katika Tamasha la wiki ya Mwananchi

“Fikiria hakuna Mwandishi wa Manara Tv wala wa chombo kingine aliyewahi kuniuliza kwa nini unasema Pacome atakuwa MVP wa Msimu huu wa 2024/25?”

“Hata yeye mwenyewe nilipomwambia kule Avic Town siku moja kabla ya Sherehe za wiki ya Wananchi, sikumuona kama alikuwa amenielewa”

“Ndio nilimwambia nakuona unashinda tuzo ya mchezaji bora msimu huu unaokuja, akacheka tu. Lakini nilishaiona miguu na akili yake kubwa Uwanjani na nikajiambia hatazuilika this season”

“Now hakuna ubishi kwamba msimu wa 2024/25 Paccome ’ Bugati ‘ anaenda kukabidhiwa Tuzo hii kubwa kabisa nchini,” aliandika Manara kwenye ukurasa wake ww mtandao wa kijamii

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *