CHE MALONE, MUSA CAMARA NA WENGINE KUPEWA THANK YOU MUDA SI MREFU

CHE MALONE, MUSA CAMARA NA WENGINE KUPEWA THANK YOU MUDA SI MREFU

Mpaka sasa kiungo Fabrice Ngoma tayari amewaaga mashabiki wa Simba baada ya mkataba wake kumalizika

Ngoma hakusubiri kupewa Thank You baada ya mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake kugonga mwamba

Mlinda lango Aishi Manula nae ni mchezaji wa pili kuondoka Simba baada ya mkataba wake kumalizika

Manula tayari amesaini kuitumikia Azam Fc kinachosubiriwa ni klabu hiyo kumtambulisha

Ukiachana na wachezaji hao, kuna orodha ya wachezaji wengine ambalo panga la Simba huenda ‘likapita nao’

Wachezaji ambao walikuwa nafasi finyu katika kikosi cha kwanza kama beki Hussein Kazi, mlinda lango Hussein Abel ni miongoni mwa wachezaji hao

Lakini pia wapo wachezaji ambao licha ya kutopata nafasi mara kwa mara, wanaweza kuhitajika baadae, hao huenda wakatolewa kwa mkopo

Hapa wachezaji kama Edwin Balua, Ladark Chasambi, Omary Omary, Ali Salim na Valentino Mashaka ni miongoni mwao

Pia ipo orodha ya wachezaji ambao wanaweza kuondoka kutokana na mahitaji ya maboresho ya kiufundi licha ya kuwa walitumika katika kikosi cha kwanza

Beki Che Malone Fondoh amemaliza mkataba lakini huenda asiongezewe mkataba mwingine Simba ikiwekeza nguvu kusaka beki mwingine wa kati huku kiungo Augustine Okejepha akiwekwa sokoni kama ilivyo kwa Steven Mukwala ambaye taarifa za ndani zimedokeza kuwa Simba imepokea ofa kwa ajili ya mchezaji huyo raia wa Uganda

Simba pia inatajwa kuwa katika mchakato wa kusajili magolikipa wawili mmoja wa ndani na mwingine wa kigeni, hiyo ikimaanisha huenda Moussa Camara nae akaachia nafasi yake

Mbivu na mbichi za usajili zitaanza kufahamika wiki ijayo kwani Simba itahitaji kukamilisha michakato yake yote ya maboresho kabla ya timu kuelekea pre-season

Squid Game (S03) Ep4

MIENDELEZO YA MUVI HIZI NA NYINGINE DOWNLOAD APP YETU👇🏻👇🏻

App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP ITAKAYOKUWEZESHA KUTAZAMA MUVI BURE

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *