BREAKING: Yanga watoa Taarifa hii kuhusu Max Nzengeli ni baada ya tetesi kuwa anaondoka Yanga

 

Klabu ya Yanga ilishafunga hesabu kwa kumuongezea mkataba kiungo wake kiraka Maxi Nzengeli raia wa DR Congo, imefahamika

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo imebainisha kuwa Maxi alisaini mkataba wa miaka miwili mwezi Mei 2025, hivyo kinachoendelea sasa mitandaoni kuhusu mustakabali wake ni propaganda tu

“Taarifa zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii ni kama propaganda ambazo waliozisambaza wanajua lengo lao, lakini ukweli ni kwamba Maxi ameshasaini mkataba wa miaka miwili,” alithibitisha mtoa taarifa kutoka Yanga.

Maxi Nzengeli amekuwa mhimili muhimu wa kikosi cha Yanga tangu alipojiunga, akionyesha uwezo mkubwa wa kucheza nafasi tofauti uwanjani kiungo, winga, na hata beki wa pembeni inapobidi.

Katika misimu yake miwili na Wananchi, amechangia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na mataji ya ligi, kombe la FA na kufika robo fainali ya CAF Champions League mwaka 2024.

Mbali na Maxi, Yanga pia imefanikiwa kuwalinda nyota wengine muhimu ambao mikataba yao ilikuwa inakaribia kuisha. Miongoni mwao ni Pacome Zouzoua, Dickson Job, na Mudathir Yahya, waliowekewa mikataba mipya kama sehemu ya mpango wa klabu kujenga kikosi imara kwa msimu ujao.

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *