ALI MAYAY NAYE ALALAMIKA KUHUSU KARIA KESI KUCHUKULIWA BMT

ALI MAYAY NAYE ALALAMIKA KUHUSU KARIA KESI KUCHUKULIWA BMT
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Ali Mayay ni miongoni mwa wagombea waliojitosa kuwania kiti cha Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Leo ndio siku ya mwisho kwa wagombea waliochukua fomu kuzirejesha ambapo Mayay ni miongoni mwa waliorejesha fomu hizo licha ya kukumbana na changamoto ya kupata wadhamini
Rais anayetetea kiti chake Wallace Karia inaelezwa amechukua ‘Endorsement’ zote na hivyo kuwafanya wagombea wengine wakose na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, waliorejesha fomu bila ‘endorsement’ wataenguliwa kwa kukosa moja ya vigezo
Mayay amesema licha ya kukosa ‘endorsement’ amerejesha fomu ili kukamilisha hatua ya kwanza ya mchakato huo wa uchaguzi
Inaelezwa wagombea ambao wamekosa ‘endorsement’ wanakusudia kufungua malalamiko BMT kupinga kanuni hiyo inayowanyima haki ya kuwa wagombea
Kanuni wanayoilalamikia ni inayohusu mgombea kukosa sifa endapo atakosa walau wadhamini/wajumbe wa 5 kwa njia ya barua
Inaelezwa wajumbe wote 47 wamemdhamini mgombea anayetetea kiti chake, Karia
